Katika hali ambayo wimbi la malalamiko ya Waislamu wapatao bilioni moja na nusu kuhusiana na vitendo vya dharau vinavyofanywa na maadui wa Uislamu nchini Marekani na kwingineko yanaendelea kushuhudiwa katika pambe mbalimbali za dunia, Mayahudi walio na misimamo ya kupindikia mipaka siku ya Jumanne walitumia vibaya kimya kinachoonyeshwa na jumuiya za kimataifa kuhusiana na suala hilo, ili kuendeleza dharau na ubezaji dhidi ya kitabu kitakatifu cha Waislamu Qur'ani, huko katika mji wa Quds.
Kufuatia kitendo cha baadhi ya Wakristo wenye misimamo ya kupindukia mipaka nchini Marekani cha kuchana na kuchoma moto Qur'ani Tukufu, baadhi ya Mayahudi walio na misimamo sawa na hiyo wanaoishi huko Jafa katika eneo la Quds Tukufu, siku ya Jumanne walichukua hatua ya kukichana kitabu hicho kitakatifu. Waislamu kadhaa walioshuhudia kitendo hicho cha udhalilishaji walishambuliwa na Mayahudi hao walipojaribu kukusanya kurasa zilizochanwa na kutupwa ardhini.
Vilevile baada ya kundi hilo lenye chuki dhidi ya Uislamu kuwashambulia Waislamu waliokuwa wakilalamikia kitendo hicho cha dharau, lilipiga nara zilizo dhidi ya Uislamu na kukariri tena vitendo vya kuikosea heshima Qur'ani. 655749