Akitoa taarifa kuhusu jambo hilo, Ali Yeral, mkuu wa jumuiya hiyo amesema kuwa kitendo kilichofanywa na baadhi ya raia wa Marekani cha kuchana na kuchoma moto Qur'ani Tukufu ni cha kitoto. Amesema hatua ya Kasisi Terry Jones ya kutaja siku ya Septemba 11, siku ya kutekelezwa mashambulio ya kigaidi nchini Marekani, kuwa siku ya kimataifa ya kuchomwa Qur'ani, ni juhudi za kasisi hiyo za kujaribu kujipatia umashuhuri kimataifa na pia kuuhusisha Uislamu na ugaidi.
Ali Yeral amesema kitendo cha kasisis hiyo muovu kimewashajiisha baadhi ya watu nchini Marekani na kwingineko duniani kubadili mtazamo wao kuhusu utukufu wa Qur'ani na hivyo kuchukua hatua ya kuibeza hadharani.
Huku akiashiria kuwa Uislamu ni dini ya amani na upendo, Yeral amesisitiza kuwa dini hii tukufu hairuhusu hata kudhuriwa wanyama na mimea. Kwa msingi huo amesisitiza kuwa kama kundi fulani la Waislamu litafanya mambo yanayokwenda kinyume na mafundisho ya dini hii tukufu, hiyo haitakuwa dalili ya kuujumuisha umma nzima wa Kiislamu kwenye kundi hilo. Amesema katika kipindi chote cha historia, kuna vita vingi ambavyo vimeendeshwa na Wakristo pamoja na Mayahudi dhidi ya Uislamu lakini Waislamu hawavinasibishi vita hivyo na Injili wala Torati, bali wamesema kuwa vita hivyo vilitokana na mitazamo mibaya ya baaadhi ya watu.
Yeral amesema mwishoni mwa taarifa hiyo kwamba anataraji vitendo kama hivyo vya ubezaji Qur'ani havitakaririwa tena na kwamba hakuna nchi yoyote itakayoshambuliwa na nyingine kwa kisingizio cha kutetea uhuru na mapambano dhidi ya ugaidi. 656546