IQNA

Mafunzo ya thamani za Qur'ani kutolewa nchini Sudan

16:33 - September 18, 2010
Habari ID: 1996260
Mafunzo ya thamani za Qur'ani yatatolewa nchini Sudan tarehe 20 hadi 22 mwezi huu Septemba chini ya usimamizi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO.
Mafunzo hayo yatahusisha Jumuiya ya Ulinganiaji wa Kiislamu na kuhudhuriwa na wataalamu kutoka nchi za Sudan, Misri, Morocco, Nigeria, Chad, Somalia na Tanzania.
Lengo la kutolewa mafundisho hayo limetajwa kuwa ni kuarifisha thamani za kimsingi za utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu, kuchunguza sababu zinazowaweka mbali Waislamu na thamani za dini hiyo na kujadili mambo yanayokwamisha mafundisho ya Kiislamu kwa mbinu za kisasa.
Vilevile duru hiyo ya mafundisho itajadili nafasi ya thamani za Kiislamu katika ustawi wa masuala ya kiroho ya Waislamu, ratiba na mipango ya kuwaelimisha Waislamu mafundisho ya dini yao, kujumuishwa thamani za Kiislamu katika mfumo wa elimu wa taifa, kutayarisha walimu wa Qur'ani na kubadilishana uzoefu kati ya wawakilishi wa nchi zinazoshiriki katika mafunzo hayo. 656811
captcha