Taarifa hiyo imesema kuwa madola ya kikoloni na kibeberu yanatumia vibaya nara ya haki za binadamu kwa ajili ya kudhamini maslahi yao haramu. Imesema, walimwengu wameanza kutambua vyema kwamba suala la haki za binadamu limekuwa likitumiwa na madola hayo kama chombo tu cha kutoa mashinikizo ya kisiasa na kiuchumi dhidi ya mataifa yanayojitawala ulimwenguni ambayo hayako tayari kufuata siasa zao za kibeberu.
Taarifa hiyo imesema kuwa kuchomwa moto Qur'ani Tukufu, kutisha, kuchochea na kuhamasisha watu kutenda kitendo hicho kiovu ni njama mpya inayotumiwa na Marekani dhidi ya maadui wake na kwamba inaweza kuchukuliwa kuwa ni utangazaji vita dhidi ya dini za mbinguni.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa Waislamu ulimwenguni wameshangazwa na kimya cha serikali ya Rais Barack Obama wa Marekani kuhusiana na wito ulio dhidi ya thamani za kiutu uliotolewa na Kasisi Terry Jones, wa kutaka kuchomwa Qur'ani Tukufu na kwamba wangali wanasubiri serikali hiyo ichukue hatua za kisheria dhidi ya kasisi huyo.
Imesema, kuchomwa moto Qur'ani na vitabu vingine vya mbinguni ni ukiukaji wa wazi wa misingi ya haki za binadamu zikiwemo mada za 19 na 130 za maazimio ya kimataifa ya haki za binadamu na vilevile mada ya 22 ya azimio la haki za binadamu za Kiislamu.
Tarifa hiyo imeonya dhidi ya kukaririwa vitendo kama hivyo na kusema kuwa kuna udharura wa kuheshimiwa matukufu ya kidini ili kulinda amani, usalama na uthabiti wa dunia. Imesisitiza kwamba kulindwa jambo hilo ni jukumu la serikali na jamii nzima ya kimataifa. 656995