IQNA

Wazayuni, waendeshaji halisi wa hujuma dhidi ya Qur'ani

23:06 - September 19, 2010
Habari ID: 1997029
Vyombo muhimu vya habari ambavyo vinamilikiwa na kuendeshwa na magenge ya Kizayuni vina matumaini ya kuanzishwa tena vita vya msalaba dhidi ya Uislamu, na kuchomwa moto Qur'ani Tukufu ni moja ya mbinu za kufikiwa lengo hilo.
Hayo yamesemwa na Muhammad Ridha Swaleh, mwandishi na mtafiti wa masuala ya Qur'ani, ambaye ameongeza kwamba Wazayuni ndio walio nyumba ya harakati za kichochezi dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi.
Amesema, waovu hao wanaomiliki mashirika na vyombo muhimu vya habari katika nchi hizo wanafanya njama hatari za kuhuisha vita vya msalaba na baadhi ya mivutano ya kihistoria kati ya Waislamu na Wakristo na hivyo kufikia lengo lao la kudumisha uadui wa kihistoria wa Mayahudi walio na taasubi za kidini dhidi ya Uislamu. Hata hivyo amesema kuwa wanafikra na wasomi huru wa Kikrito wanapinga vikali njama hiyo ya Wazayuni na ndio maana wakawa wamejitokeza wazi kulaani tukio la hivi karibuni la kuchomwa moto Qur'ani Tukufu nchini Marekani.
Bwana Swaleh amesema kuwa kasi ya kuenea mafundisho ya Kiislamu katika nchi za Magharibi ni moja ya sababu kuu ambazo zimepelekea baadhi ya watu wenye misimamo ya kiuadui dhidi ya dini hii tukufu kuchukua hatua ya kuchoma moto Qur'ani. Amesema, hata kama kuna uzoefu wa nchi za Magharibi kufanya uadui na njama dhidi ya Uislamu lakini katika zama hizi njama hizo zimechukua mkondo maalumu na wa siri kiasi kwamba si rahisi kufahamika na kila mtu. Amesema, ni wazi kuwa watu wa Magharibi wanaodai kuwa wamestaarabika na kuheshimu misingi ya demokrasia na uhuru wa kusema, ndio haohao wanaochukua hatua za chuki na uadui dhidi ya mafundisho ya Qur'ani na kwa hivyo ni wazi kuwa watu hao ni majahili wa zama hizi.
Bwana Swaleh amesisitiza kwamba watenda jinai hiyo ya kiutamaduni ni majahili hata kuwaliko washirikina wa zama za ujahili waliokuwa wakiweka pamba kwenye masikio yao ili wasije wakasikia ujumbe wa Qur'ani na maneno ya Mtume Mtukufu (SAW). 657017
captcha