IQNA

al Azhar yavunja Kamati ya Mazungumzo kati ya Dini Mbalimbali

0:42 - September 20, 2010
Habari ID: 1997236
Sheikh wa al Azhar Ahmad al Tayyib amevunja Kamati ya Mazungumzo kati ya Dini Mbalimbali.
Mshauri wa Sheikh wa al Azhar Mahmoud Azb amesema kuwa kituo kipya kitaanzishwa kwa ajili ya kusimamia mazungumzo ya maulama wa al Azhar na wasomi wa Magharibi na kwamba kazi kubwa ya kituo hicho itakuwa kubuni njia za kuimarisha ushirikiano kati ya maulama wa al Azhar na wasomi wa tamaduni nyingine.
Amesema kituo hicho kipya kitatilia maanani thamani za pamoja za kibinadamu kama haki, uadilifu, usawa, utukufu wa mwanadamu na kupambana na ujinga, umaskini na maradhi. Amesisitiza kuwa misingi na thamani hizo zinapatikana kwa wafuasi wa dini na tamaduni zote, na Uislamu umehimiza suala la mazungumzo kuhusu masuala hayo.
Mahmoud Azb ameesema kuwa kituo hicho kitafanya mazungumzo na wanafikra wa Kikristo na Kiyahudi lakini hakitafanya mazungumzo na Wazayuni na Wayahudi wenye misimamo ya kupindukia. Hii ni kwa sababu Wazayuni wametwaa na kukalia kwa mabavu ardhi za mataifa mengine na kukiuka heshima na haki za binadamu. 658064
captcha