Lengo la kongamano hilo limetajwa kuwa ni kufanya mazungumzo baina ya wanafikra wa Kiislamu na wasiokuwa wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali duniani kuhusu maudhui za 'Waislamu na thamani za Magharibi', 'sababu za kuongezeka hujuma dhidi ya Uislamu', 'historia ya Uislamu katika nchi za Magharibi' na 'nafasi ya vyombo vya habari katika kustawisha utamaduni wa kuvumiliana'.
Kongamano hilo la kimataifa litahudhuriwa na Abdul Ilah bin Arafa, mtaalamu wa masuala ya utamaduni na mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu ISESCO. 660467