Kwa ushirikiano wa Muungano wa Kituruki na Kiislamu unaofungamana na Taasisi ya Dini ya Uturuki DITIB, Wizara ya Wahamiaji ya Ujerumani ina lengo la kutoa mafunzo maalumu ya maarifa na lugha ya Kijerumani kwa maimamu wa swala za jamaa katika jimbo la Niedersachsen kuanzia mwezi ujao wa Oktoba.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Uturuki la Jahan, mafundisho kama hayo tayari yametolewa kwa maimamu wa misikiti katika miji ya Cologne, Frankfurt na Nuremburg. Lengo la mafundisho hayo limetajwa kuwa ni kusaidia kuwaunganisha Waislamu wa Ujerumani katika jamii ya Kikristo ya nchi hiyo.
Tokea sasa, maimamu hao baada ya kusoma lugha ya Kijerumani wataweza kuwavutia Waislamu waliozaliwa nchini Ujerumani ambao hawajua Kiarabu misikitini na hivyo kuzuia kudhihiri makundi mawili tofauti ya Waislamu walio wachache nchini humo.
Mbali na kufundishwa lugha ya Kiarabu, maimamu hao pia watasomeshwa masomo yanayohusiana na utamaduni na mila za Wajerumani, kufahamishwa mashirika na taasisi rasmi za masomo, wawakilishi wa dini tofauti na njia za kuimarisha ushirikiano na wafuasi wa dini nyinginezo.
Masomo hayo yanatazamiwa kuenezwa katika majimbo mengine ya Ujerumani. 661521