Mashindano hayo yameandaliwa na Idara Kuu ya Vijana na Michezo kwa ushirikiano wa Idara ya Masomo ya Qur'ani Tukufu ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Kuwait.
Gazeti la nchi hiyo la al-Anba limekuwa likifuatilia kwa karibu mashindano hayo ambayo yanafanyika katika eneo la al-Mubarak na ambayo yanasimamiwa na kamati 10 kwa ajili ya washindani wanaume na kamati 5 kwa asili ya washindani wanawake.
Wasimamizi wa mashindano hayo wanasema kuwa yanafanyika kwa lengo la kuwatayarisha vijana wa Kuwait kuhifadhi Qur'ani.
Mashindano hayo yaliyoanza Jumamosi alasisiri yamepangwa kuendelea hadi siku ya Alkhamisi tarehe 30 Septemba. 663602