Mkutano huo utakaomaliza kazi zake kesho unawakutanisha pamoja maafisa wa ngazi za juu wa nchi 29 zikiwemo Algeria, Uganda, Msumbiji, Sierra Leone, Syria, Saudi Arabia, Comoro na Djibout.
Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kama FAO, UNDP, WFP na Baraza la Ushirikiano wa Nchi za Ghuba ya Uajemi (CCASG) pia wanahudhuria mkutano huo.
Mkutano huo unajadili hali ya chakula duniani hususan katika nchi za Kiislamu na suala la kudhamini chakula kwa ajili ya watu milioni 925 wanaosumbuliwa na njaa na umasikini duniani.
Masuala mengine yanayojadiliwa katika mkutano huo wa kimataifa ni taathira za mdororo wa kiuchumi kwa sekta ya chakula katika nchi za Kiislamu, udharura wa kutiliwa maanani uzalishaji wa chakula katika nchi wanachama wa OIC na kuimarisha miundombinu katika nchi za Kiislamu. 664578