Kwa mujibu wa tovuti ya arabic.business.maktoob, kikao hicho kitafanyika Disemba 12 hadi Disemba 16 kwa lengo la kukurubisha pamoja mitazamo na malengo ya nchi za Kiislamu kuhusiana na masuala ya kiuchumi. Maonyesho ya kimataifa ya Kiislamu pia yatafanyika pambizoni mwa kikao hicho.
Kikao hicho kinafanyika kwa ushirikiano wa Baraza Kuu la Utalii la Saudi Arabia, Benki ya Maendeleo ya Kiislamu, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu na Idara ya Biashara na Viwanda ya Kiislamu.
Kukurubisha pamoja mitazamo na malengo ya kiuchumi ya nchi wanachama wa jumuiya ya OIC ni moja ya mambo muhimu yatakayojadiliwa katika kikao hicho cha siku tano. 663897