Kwa mujibu wa gazeti la Chicago Tribune, chuo hicho kilichofunguliwa rasmi miongo kadhaa iliyopita mara hii kitaanza kwa kuandaa mkutano maalumu na kisha kuendelea na shughuli zake za kawaida za masomo.
Chuo hicho ambacho kiko karibu na ziwa la Michigan kilifunguliwa mwaka 1981 na tokea wakati huo hadi sasa uongozi wake umebadilika mara kadhaa. Licha ya hayo, chuo hicho hakijapata kibali rasmi cha kuendesha shughuli zake na kwa hivyo wanachuo wanaohitimu masomo yao huko huwa hawapewi vyeti rasmi vinavyotambuliwa na serikali ya Marekani.
Chuo hicho ambacho kinaendeshwa na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC hadi sasa kimesajili wanafunzi 50 ambao wanatazamiwa kuanza masomo yao katika kipindi cha wiki mbili zijazo. 664978