IQNA

Mahmoud Abbas ameshindwa kufuatilia malengo ya taifa la Palestina

11:26 - September 29, 2010
Habari ID: 2003804
Matokeo ya hivi karibuni ya uchunguzi wa maoni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel yanathibitisha kwamba Mahmoud Abbas, Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameshindwa kufuatilia na kulinda malengo ya taifa la Palestina.
Shirika huru la habari la Palestina SAMA, ndilo lililofanya uchunguzi huo wa maoni kufutia mazungumzo ya moja kwa moja ya mapatano kati ya utawala wa Kizayuni na Mahmoud Abbas huko nchini Marekai na Misri.
Wapalestina wapatao 7,891 walishiriki katika uchunguzi huo wa maoni uliochukua wiki moja. Asilimia 72.1 ya washiriki walisema kuwa Mahmoud Abbas hawezi kulinda malengo ya Wapalestina kupitia mazungumzo hayo. Ni asilimia 26.5 tu ndio waliosema kuwa anaweza kulinda maslahi na malengo hayo kupitia mazungumzo na Wazayuni. Asilimia 1.1 hawakujibu maswali waliyoulizwa kuhusu jambo hilo.
Asilimia 4.37 ya Washiriki ni wakaazi wa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan, asilimia 45.5 wakazi wa Ukanda wa Gaza na waliosalia ni wakazi wa nchi nyinginezo.
Tunakumbusha hapa kuwa duru mpya ya mazungumzo ya mapatano kati ya Wazayuni na Mahmoud Abbas ilianza Septemba Pili ambapo hadi sasa hakuna natija yoyote ya maana iliyopatikana kwenye mazungumzo hayo. 665352
captcha