Batalioni ya Quds ambayo ni tawi la kijeshi la harakati ya kupigania uhuru wa Palestina ya Jihad Islami imetoa wito wa kuanzishwa mapambano mapya ya Intifadha kwa lengo la kufanikisha mpango wa kitaifa wa Palestina. Wito huo umetolewa kwa ajili ya kuadhimisha kutimia miaka kumi tangu kuanza Intifadha ya Pili.
Taarifa iliyotolewa na Batalioni ya Quds imesema kuwa viongozi 654 wa mapambano ya Intifadha wa Batalioni ya Quds wameuawa shahidi tangu Intifadha ya Pili ianze tarehe 28 Septemba mwaka 2000. imeongeza kuwa makombora na maroketi 3205 yamefyatuliwa na Batalioni ya Quds dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi na operesheni 126 za kujitolewa muhanga zimetekelezwa na wapiganaji wa Jihadi Islami katika maeneo mbalimbali ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Imesema kuwa operesheni hizo zimepelekea kuangamizwa Wazayuni 199.
Msemaji wa Batalioni ya Quds Abu Ahmad amesema kuwa batalioni hiyo itaendeleza mapambano ya jihadi dhidi ya Wazayuni maghasbu.
Kamati ya Harakati ya Mapambano ya Wananchi pia imetoa taarifa kwa mnasaba wa kutimia miaka kumi tangu kuanza mapambano ya Intifadha ya Pili kisisitiza juu ya udharura wa kudumishwa mapambano hadi kukombolewa ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestina.
Taarifa hio imesisitiza kwamba kufanya mazungumzo na adui Mzayuni ndio wenzo unaotumiwa na adui huyo na matokeo yake yanawanufaisha maadui wa taifa la Palesina.
Kundi hilo limewataka watetezi wa uhuru kote duniani kutekeleza wajibu wao kuhusu Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu. 665380