Kwa mujibu wa tovuti ya Prlog maonyesho hayo yatafanyika kwa shabaha ya kuarifisha vyakula na viwanda vinavyozalisha bidhaa halali, kuandaa mazingira ya kuimarishwa shughuli za utengenezaji wa bidhaa halali pamoja na sekta nzima inayohusiana na uzalishaji wa bidhaa hizo.
Kamati inayosimamia bidhaa halali nchini Uingereza HMC ambayo inawajumuisha maulama na wanazuoni kutoka nchi tofauti na iliyoasisiwa mwaka 2003 ndiyo inayoandaa na kusimamia maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yataanza saa sita hadi saa moja jioni kwa wakati wa Uingereza na wazalishaji pamoja na watu wanaojishughulisha na uuzaji na ununuzi wa vyakula pamoja na bidhaa halali watapewa fursa ya kuonyesha bidhaa zao katika maonyesho hayo. 665559