Ayatullah Muhammad Ali Tas’khiri ameyasema hayo katika ufunguzi wa kongamano la hija nchini Indonesia na kuongeza kuwa hija ina malengo mawili makuu ambayo ni kumwabudu Mwenyezi Mungu Mmoja na kujiepusha na masanamu, suala ambalo lina umuhimu mkubwa.
Akihutubia kongamano hilo lililopewa jina la “Faida za Hija katika Kuimarisha Mshikamano na Umoja wa Waislamu”, Ayatullah Tas’khiri amesema kuwa hija ni miongoni mwa malengo muhimu ya Kiislamu na haji ana nafasi kubwa na aali na kwamba anapaswa kufanya jitihada za kulinda nafasi hiyo.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu amesisitiza juu ya udharura wa kutumiwa vyema ibada ya hija kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu na kudhihirisha nguvu ya umma wa Kiislamu.
Mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika masuala ya hija pia amehutubia kongamano hilo nchini Indonesia akisema kuwa ustawi na kasi ya kuenea Uislamu duniani umewatia kiwewe viongozi wa nchi za Magharibi ambao wameanza kupanga njama za kukabiliana na dini hiyo.
Qadhi Asghari amesema umoja na mshikamano wa nchi za kiislamu ni miongoni mwa njia bora za kukabiliana na hujuma zinazofanywa na nchi za Magharibi dhidi ya Uislamu. :667886