Mashindano hayo ambayo yaliwashirikisha washindani 50, yamefanyika katika nyanja za kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 15 na juzuu saba.
Sherehe za kutunukiwa zawadi washindi zilihudhuriwa na Mufti wa Burundi Shaban Umar na wasomi na shakhsia wengine wa Kiislamu nchini humo.
Mkuu wa kamati ya majaji wa mshindano hayo ya Qur'ani Shabani Fodo ametoa hotuba akieleza matukufu ya kuhifadhi Qur'ani na akaishukuru Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani kwa kufanikisha mashindano hayo. 668295