Swalahuddin al Barduweil ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Hamas amesema kuwa hujuma hiyo imefanyika kwa ruhusa ya viongozi wa utawala haramu wa Israel kwa lengo la kuweka wazi fikra kwamba Wapalestina hawana nafasi katika ardhi hiyo.
Al Barduweil amezikosoa nchi za Kiarabu kwa kunyamazia kimya vitendo vya kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu na kuwataka wafanye jitihada za kuokoa matukufu ya Kiislamu ya Palestina kutoka kwenye makucha ya Wazayuni maghasibu.
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini ya Palestina pia imelaani vikali kitendo cha walowezi wa Kizayuni cha kuchoma moto msikiti wa al Anbiyaa katika Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan na imetahadharisha juu ya hatua za Wazayuni za kuvuruga amani na utulivu katika ulimwengu wa Kiislamu.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu kitendo cha walowezi wa Kizayini cha kuchoma moto msikiti huo katika kijiji cha Bait Fajjar.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kitendo hicho za Wazayuni kimefanyika baada ya mfululizo wa mashambulizi yaliyolenga misiki, raia na mali za Wapalestina.
Watu walioshuhudia wamesema kuwa Jumatatu ya jana tarehe 4 Oktoba walowezi sita wa Kizayuni walishambulia msikiti wa al Anbiyaa na kuchoma moto sehemu moja ya msikiti na nakala 15 za kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 668841