Ekmeleddin Ihsanoglu amelaani shambulizi lililofanywa na Wayahudi wenye misimamo ya kufurutu mipaka dhidi ya msikiti wa kijiji cha Bait Fajjar huko kusini mwa Bait Laham na kuchoma moto msikiti huo na akaongeza kuwa kitendo hicho kinakiuka sheria za kimataifa.
Anesema kuwa kuvamia msikiti, kuchoma moto nakala za Qur'ani na kuandika maneno ya dharau katika kuta zake ni kukiuka uhuru wa dini na kuvunjia heshima matukufu ya kidini.
Katibu Mkuu wa OIC amesema kuwa kitendo hicho cha Wayahudi wanaoishi katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina kinavuruga amani na utulivu wa eneo hilo.
Prf. Ihsanoglu ameitaka pia jamii ya kimataifa iulazimishe utawala wa Kizayuni wa Israel kuzuia vitendo kama hivyo na kusitisha ukiukaji wa haki za wananchi wanaokandamizwa wa Palestina. 668815