IQNA

Mfaransa akosea heshima Qur'ani Tukufu

17:02 - October 05, 2010
Habari ID: 2007216
Katika hali ambayo vitendo vya dhrau dhidi ya Qur'ani Tukufu vingali vinaendelea katika nchi za Magharibi kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza na fikra, Mfaransa mmoja ameweka kwenye mtandao wa intaneti picha za kuchanwa kitabu hicho kitakatifu.
Mfaransa huyo mkazi wa mji wa Strasbourg ameweka picha hizo za video zinazoonyesha kuchanwa kwa Qur'ani Tukufu kwa muda wa saa nzima katika hali ambayo ulimwengu bado unatoa radiamali kuhusiana na kitendo cha chuki dhidi ya Uislamu cha kuchanwa na kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani.
Abdul Aziz Shukri, mwakilishi wa msikiti mkuu wa Strasbourg ambaye amemshtaki muhusika wa kitendo hicho katika idara ya polisi amesema kwamba iwapo watu watakaa kimya mbele ya kitendo kama hicho watakuwa wamewafungulia mlango watu wengine waovu kutekeleza vitendo vya dharau dhidi ya matukufu ya dini nyinginezo za mbinguni. 668615
captcha