IQNA

Kikao cha kimataifa cha Qur'ani Tukufu kufanyika Malaysia

13:04 - October 07, 2010
Habari ID: 2008206
Kitengo cha Qur'ani na Hadithi cha Chuo Kiku cha Malaya nchini Malaysia kimepanga kuandaa kikao cha kwanza cha kila mwaka cha kimataifa kitakachojadili Qur'ani Tukufu, kikao ambacho kimepangwa kufanyika mwezi Januari mwakani.
Kikao hicho kinaandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Qur'ani cha Chuo cha Utafiti wa Kiislamu cha Malaya kwa madhumuni ya kunyanyua kiwango cha utafiti wa chuo hicho kuhusiana na Qur'ani Tukufu na kuwashirikisha zaidi wanachuo wa chuo hicho katika vikao vya kielimu vya kimataifa. Kuandaliwa uwanja wa kushirikiana wanachuo na watafiti wa Qur'ani, kualikwa wataalamu na wanafikra wa Kiislamu kutalii Qur'ani na kutumiwa teknolojia ya kisasa katika kuendeleza na kueneza mafundisho ya Qur'ani duniani, kuimarisha mbinu za utafiti wa Qur'ani na tarjumi pamoja na tafsiri ya kitabu hicho kitakatifu ni malengo mengine ya kuandaliwa kikao hicho. Kikao hicho kimepangwa kufanyika tarehe 11 na 12 za mwezi Januari. 669588
captcha