IQNA

Masomo ya kuhifadhi Qur'ani yaanza Imarati

13:48 - October 09, 2010
Habari ID: 2008918
Masomo ya kuhifadhi na tajwidi ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya wanawake yameanza leo katika Kituo cha Qur'ani cha al Atrijah katika mji wa Ajman kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu.
Afisa anayeshughulikia masuala ya habari wa Kituo cha Qur'ani cha al Atrijah Maha al Jahuri amesema kuwa masomo hayo yanahudhuriwa na wanafunzi 623 wa kike na yataendelea kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Ameongeza kuwa katika kipindi hicho wanafunzi hao pia watapata masomo ya iijazul Qur'ani (muujiza wa Qur'ani), ufahamu wa aya za mutashabihat, utambuzi wa sura za Qur'ani na visa vinavyohusiana na sura hizo.
Maha al Jahuri amesema kuwa wanawake waliochaguliwa kushiriki katika masomo hayo walishinda mtihani uliosimamiwa na kamati ya tahmini iliyojumuisha walimu wa Kiuo cha Qur'ani cha al Atrijah. 670786

captcha