IQNA

Vikao vya Maarifa ya Qur'ani vyaanza nchini Uturuki

15:17 - October 11, 2010
Habari ID: 2010770
Vikao vya Maarifa ya Qur'ani vimeanza huko Istanbul nchini Uturuki kwa udhamini wa Kituo cha Utamaduni cha Kizazi cha Qur'ani.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islamiyonelis, vikao hivyo vitakuwa vikifanyika mara moja kila baada ya wiki mbili, kama ilivyofanyika mwaka uliopita.
Vikao hivyo vitakuwa vikifanyika siku ya Jumamosi katika kituo cha Utamaduni cha Kizazi cha Qur'ani ambapo masuala mbalimbali yanayohusiana na maarifa ya Qur'ani yatajadiliwa na wahadhiri na wasomi mashuhuri wa Kiislamu.
Kikao cha kwanza kilianza hapo siku ya Jumamosi iliyopita ambapo suala la nafasi ya tarjumi za Qur'ami katika ufahamu sahihi wa maneneo ya Mwenyezi Mungu kwenye Qur'ani lilijadiliwa. Kikao kijacho cha Maarifa ya Qur'ani kitafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 Oktoba. 672292
captcha