Shughuli ya kufunguliwa tena msikiti huo mkongwe imehudhuriwa na Sayyid Salih al Haidari ambaye ni mkuu wa Taasisi ya Wakfu wa Shia nchini Iraq na shakhsia mbalimbali wa kidini na kielimu wa mji mtakatifu wa Najaf.
Mkuu wa kitengo cha utafiti cha haram ya Imam Ali (as) Mudhaffar Mahbuba amesema kuwa msikiti huo mkongwe una umri wa miaka 1000 na ulipuuzwa na kutelekezwa katika kipindi kirefu cha utawala ulioondolewa madarakani wa dikteta Saddam Hussein.
Amesema kuwa kitengo cha masuala ya uhandisi cha haram tukufu ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) kimekarabati msikiti huo kwa gharama ya dinari milioni tatu za Iraq baada ya kufanya utafiti kamili na kwamba msikiti huo sasa uko tayari kupokea wasomi na watu mbalimbali kwa ajili ya ibada ya swala. 672774