IQNA

Masomo ya Qur'ani na Uislamu yafanyika Qatar

13:47 - October 13, 2010
Habari ID: 2012016
Taasisi ya Utamaduni ya as-Sheikh Id ya nchini Qatar kwa ushirikiano wa Kituo cha Elimu ya Qur'ani na Sunna cha Saudi Arabia, imeandaa masomo ya Qur'ani na Uislamu ambayo yamepangwa kuanza hivi karibuni nchini humo.
Muhammad Abdallah As-Sai, mkuu wa idara ya ratiba za masomo ya kituo cha as-Sheikh Id amesema kuhusiana na suala hilo kwamba masomo hayo yamepangwa kuanza siku ya Jumapili tarehe 17 Oktoba. Amesema, masomo hayo ambayo yataendelea kwa kipindi cha miaka miwili yatakuwa yakifanyika siku za Jumapili, Jumatatu, Jumanne na Jumatano za kila wiki.
Amesema waalimu mashuhuri wamechaguliwa kuendesha shughuli hiyo ambapo masomo muhimu zaidi yatakayofundishwa ni pamoja na tafsiri ya Qur'ani, elimu ya Qur'ani, tajweedi, fiqhi na hadithi, fiqhi na nahau, usuul fiqhi, elimu ya hadithi, kanuni za fiqhi, fiqhi na sira, madhebu na kidini na madhehebu ya kiitikadi.
Khalil bin Muhammad az-Zeir, mkurugenzi mwandamizi wa taasisi hiyo amesema kwamba tayari shughuli ya uandikishaji wa majina ya washiriki wa masomo hayo imeanza na kwamba watakaohitimu watapewa cheti cha diploma ya masomo ya Kiislamu.
Wakuu wa taasisi hiyo wanasema kuwa lengo la kuanzishwa masomo hayo ni kuimarisha imani, thamani za kiutu, maadili na ufahamu wa sheria za Kiislamu katika jamii. 673867
captcha