Masomo hayo ya hija tamatu' ambayo ni mahsusi kwa wakaazi wa mkoa uliotajwa yataendeshwa na wasomi pamoja na wanazuoni wa Kishia wa Saudi Arabia.
Wanafunzi wa masomo ya kidini na wataalamu wa sheria na kanuni za usomaji Qur'ani wanashiriki katika utekelezaji wa ratiba hiyo ambapo watawafundisha washiriki namna ya kusoma kwa njia sahihi Qur'ani Tukufu na dua.
Masomo hayo ambayo yatawashirikisha wanawake na wanaume yatachukua muda wa wiki nne. 674295