IQNA

Demokrasia imetolewa katika Qur’ani

14:39 - October 16, 2010
Habari ID: 2013608
Jamii za nchi za Magharibi zinatumia demokrasia kwa maana tata na pengine isiyofahamika vyema.
Hayo yamesema na Nawar al Hussaini, mtafiti na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha al Amira Sumayya cha Jordan na kuongeza kuwa istilahi ya demokrasia katika ulimwengu wa Kiislamu tofauti na ulimwengu wa Magharibi inaeleweka vyema, kwani maana ya yake imetolewa katika Qur’ani na sheria za Kiislamu.
Nawar al Husseini ambaye alikuwa akihutubia kongamano la ‘Maana ya Demokrasia katika Uislamu na Uhusiano wake na Magharibi’ huko nchini Uswisi amesema kuwa dini ya Kiislamu ambayo inategemea msingi wa mashariano yanayodhamini haki za watu wote wa jamii, imewasilisha maana ya wazi zaidi kuhusu demokrasia.
Amesema kuwa demokrasia ya huko Magharibi imebuniwa na wanadamu na kwa msingi huo inaweaza kufasiriwa na kubadilishwa kwa kutegemea mambo mbalimbali, lakini demokrasia katika Uislamu imesimama juu ya misingi na thamani ambazo marejeo yake ni dhati ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kongamano la Maana ya Demokrasia katika Uislamu na Uhusiano wake na Magharibi lilianza kazi zake Jumatano tarehe 13 Oktoba na kumalizika jana Ijumaa. Kongamano hilo limehudhuriwa na wasomi na wanafikra wa Kiislamu kutoka nchi za Uswisi, Marekani, Ujerumani, Austria, na nchi za Asia, Afrika na America ya Latini. 675400
captcha