Kwa mujibu wa tovuti ya The Boston Channel Kasisi Hank Price, ambaye ni mtaalamu na mtafiti wa Kimarekani aligundua Qur'ani hiyo katika kanisa la Uneversalist alipokuwa akitafuta vitabu vya kale katika maktaba ya Askofu David Sgoud ambaye alihudumia kanisa hilo yapata miaka 300 iliyopita. Price ameashiria kwamba nuskha hiyo ni tarjuma ya Qur'ani iliyochapishwa mwaka 1759, mwishoni mwa mapinduzi ya Marekani na katika kipindi ambacho hakuna Muislamu yoyote aliyekuwa akiishi katika jimbo la Massachusetts. Amesema Askofu Sgoud alinunua kitabu hicho kwa lengo la kukitwalii. Amesema kugunduliwa kwa Qur'ani hiyo katika maktaba iliyotajwa kuna umuhimu kwa kutilia maanani kwamba jambo hilo linathibitisha kuwa mafundisho ya Mtume Mtukufu (saw) yalifika katika eneo hilo zaidi ya karne mbili zilizopita. 675807