Tamasha hiyo inasimamia na Haram Tukufu ya Imam Hussein kwa ushirikiano na Idara ya Wakfu ya Shia.
Tamasha hiyo ya Wiki ya Qur'ani inafanyika katika uwanja wa haram tukufu ya Imam Hussein katika mji wa Karbala ikiwashirikisha wawakilishi wa nchi 20 na inajumuisha shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kongamano la utafiti wa Qur'ani, kukutanisha pamoja taasisi zinazojihusisha na masuala ya kitabu hicho kitakatifu na kuwaenzi wasomaji Qur'ani wa kale wa Iraq.
Karim Yasir, kari wa Kituo cha Sayansi ya Qur'ani cha Idara ya Wakfu ya Shia ya Iraq amesema kuwa mashindano ya Qur'ani yatafanyika pia katika tamasha hiyo na washindi wataiwakilisha Iraq katika mashindano ya kimataifa.
Ameongeza kuwa washiriki wengi wa mashindano hayo ni wasomaji na mahafidhi mashuhuri wa Iraq ambao wameshiriki katika mashindano mengi ya kimataifa katika nchi mbalimbali. 676422