IQNA

Msahafu unaosema wazinduliwa nchini Qatar

11:40 - October 19, 2010
Habari ID: 2015736
Msahafu unaosema umezinduliwa nchini Qatar kwa hima ya Kitengo cha Utamaduni cha Taasisi ya Huduma za Kibinadamu (RAF).
Mkurugenzi wa Kitengo cha Shughuli za Kiutamaduni cha Jumuiya ya Huduma za Kibinadamu RAF Fahad Jam’an al Qahtani amesema kuwa msahafu huo umetayarishwa kwa lengo la kutoa elimu ya tajwidi ya Qur’ani na kueneza utamaduni wa Kiislamu hususan utamaduni wa kuhifadhi na kusoma na Qur’ani kati ya Waislamu.
Al Qahtani amesema kuwa msahafu huo unajumuisha kiraa mbalimbali za Qur’ani tukufu zikiwemo za Hafs, Warsh, Qalun, al Duri na kadhalika na hadithi za Mtume Muhammad (saw) zinazohusiana na Qur’ani. Msahafu huo pia unajumuisha kitabu cha Asbabu al Nuzul cha Suyuti.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni cha Taasisi ya Huduma za Kibinadamu ya Qatar (RAF) amesema kuwa msahafu huo wenye thamani kubwa utatoa huduma kubwa katika kueneza utamaduni wa Qur’ani kati ya matabaka mblimbali ya jamii ya Kiislamu na kulea kizazi cha Waislamu kwa mujibu wa thamani za neno la Mwenyezi Mungu, kuuamsha umma wa Kiislamu na kutumia maarifa ya Qur’ani kwa ajili ya kufikia kilele cha maendeleo. 678148
captcha