Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, takribani wasomi na wanafikra 160 wa dini tatu za Uislamu, Ukristo na Uyahudi kutoka nchi 58 duniani wanashiriki katika kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Mazungumzo ya Dini mjini Doha.
Dr. Aisha Yusuf al-Mannai Mkuu wa Kitivo cha Masomo ya Kidini na Utafiti wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Qatar ambaye pia ni mwanachama wa Baraza la Ushauri la Kituo cha Kimataifa cha Mazungmzo ya Dini mjini Doha amesema kuwa, ' katika siku ya kwanza ya kongamano hilo washiriki walijadili nafasi ya familia ya malezi ya kidini, akhlaqi za kizazi kipya, athari za talaka katika kudhoofisha thamani za kidini na akhlaqi za watoto na vile vile malezi ya watoto kwa mujibu wa kustahamiliana. Amesema katika siku yake ya pili kongamani hilo litajadili masiala kama vile nafasi ya vituo vya elimu, kijamii na vyombo vya habari katika malezi ya kidini ya vizazi vijavyo, n.k.
Dr Aisha Yusuf al-Mannai amesema mijadala ya siku ya mwisho ya kikao hicho itahusu masuala kama vile mtazamo wa vijana kuhusu mazungumzo ya dini mbalimbali na nafasi ya dini katika malezi ya vizazi vijavyo.
678895