Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Naheed Nenshi amechaguliwa kuwa meya wa mji wa Calgary licha ya kuwepo ushindani mkali katika mji huo ambao ni mgome ya wahafidhina mbali na kuwa eneo anakotoka Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper.
Naheed Nenshi ambaye ana umri wa miaka 38 alimshinda mgombea aliyekuwa akiungwa mkono na waziri mkuu huyo.
Baada ya kuchaguliwa Nenshi Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Canada Dtk. Ziyad Delic amesema Waislamu hukumbana na vizingiti vingi katika njia ya kufika vyeo vya juu katika nchi zisizo za Kiislamu. Amesema wakati umefika kwa Waislamu Canada kuweza kueneza thamani za Kiislamu.
Naheed Nenshi ambaye alizaliwa Toronto ni mtoto wa mhajiri kutoka Tanzania. Alihama kutoka Toronto na kuelekea Calgary kisha akaelekea Chuo Kikuu cha Harvard Marekani kupata masomo ya Juu.
Mjii wa Calgary uko kusini mwa mkoa wa Alberta nchini Canada na ni moja kati ya maeneo muhimu ya kiuchumi nchini humo. 679142