IQNA

Hamburg kutambua rasmi dini ya Kiislamu

13:05 - October 21, 2010
Habari ID: 2017024
Kuwepo jamii kubwa ya Waislamu nchini Ujerumani hususan Waislamu wa mji wa Hamburg wanaounda asilimia 5 ya wakazi milioni 1.7 wa mji huo kunaonyesha kwamba Uislamu umeoana na utamaduni wa nchi hiyo.
Viongozi na wanasiasa wa Kiislamu wa Ujerumani wanatazamia kuwa Hamburg inakaribia kutambua rasmi dini tukufu ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa kituo cha Islam Today, viongozi na wanasiasa wa Kiislamu wa Ujerumani wanaamini kwamba japokuwa mpango wa kutambuliwa rasmi dini ya Kiislamu unakaribia kutimia lakini mivutano iliyopo nchini Ujerumani kuhusu dini ya Kiislamu na mabadiliko ya kisiasa nchini humo huenda yakatatiza mwenendo wa kupasishwa suala hilo.
Zakaria Altog mkuu wa Jumuiya ya Kituriki na Kiislamu ya Taasisi ya Dini ya Uturi tawi la Hamburg ambayo ni jumuiya kubwa zaidi ya Kiislamu nchini Ujerumani anasema umuhimu wa mpango huo kwa Waislamu wa Hamburg unatokana na ukweli kwamba unawahesabu Waislamu kuwa ni sehemu ya jamii ya Ujerumani.
Ameongeza kuwa kupasishwa mpango huo kutawawezesha Waislamu wa Ujerumani kupewa haki zao za kiraia.
Siku chache zilizopita Rais wa Ujriumani alitangaza waziwazi kuwa Waislamu ni sehemu ya utamaduni wa Ujerumani. 679084
captcha