IQNA

Kongamano la Kimataifa la "Huduma kwa Mwanadamu" laanza Uturuki

13:41 - October 23, 2010
Habari ID: 2017357
Kongamano la Kimataifa la 'Huduma kwa Mwanadamu' limeanza tarehe 22 Oktoba mjini Istanbul nchini Uturuki na kuhudhuriwa na zaidi ya nchi 40.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo la siku mbili limefanyika kwa ushirikiano wa chuo cha Al Maahad al Aali al Islami Hyderabad cha India na Jumuiya ya Maarifat ya Uturuki. Inatazamiwa kuwa wasomi na maulama 300 wa Kiislamu wanahudhuria kongamano hilo ambalo linakusudia kuchunguza nafari ya Uislamu katika kumpa mwanadamu thamani.
Kati ya wasomi waliowasilisha makala zao katika kongamano hilo ni pamoja na Abdullah Bin Bihh Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulama Waislamu, Farouq Hamad Mhadhiri wa Sayansi ya Hadithi kutoka Chuo Kikuu cha Rabat Morocco, Mohammad Awamah kutoka Saudi Arabia, Sheikh Khalid Seifullah Rahmani Mkuu wa Jumuiya ya Fiqhi ya India na Usama Rafai Mufti wa eneo la Akar la Lebanon. 679997
captcha