IQNA

'Wiki ya Kuufahamu Uislamu' katika Chuo Kikuu cha Missouri Marekani

10:09 - October 24, 2010
Habari ID: 2018058
'Wiki ya Kuufahamu Uislamu' katika Chuo Kikuu cha Missouri nchini Marekani inatazamiwa kufanyika kati ya tarehe 25-28 Oktoba kwa himaya ya Jumuiya ya Wanachuo wa Kiislamu wa chuo hicho.
Kwa mujibu wa tovuti ya Columbia Missourian, 'Wiki ya Kuufahamu Uislamu' imeandaliwa ili kuiarifisha dini tukufu ya Kiislamu.
'Wiki ya Kuufahamu Uislamu' hufanyika katika majira ya machipuo. Hata hivyo kutokana na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu hasa upinzani wa kujengwa Msikiti mjini New York na vile vile kuchomwa moto Qur'ani na misikiti imeamuliwa kuandaa hafla hiyo mapema zaidi.
Mahir Khan Mkuu uhusiano wa umma wa Jumuiya ya Wanachuo Waislamu katika Chuo Kikuu cha Missouri amesema, 'tunataka kuwafunza Wamarekani maana halisi ya Uislamu hasa kutokana na kuwa wanapata taswira potofu kuhusu Uislamu wakitizama mikanda ya sekunde 30katika talevisheni za Fox News au CNBC'.
Katika siku ya kwanza hafla hiyo itajadilia suala la 'Waislamu katika Vyombo vya Habari'. Siku ya pili kutakua filamu yenye anwani ya 'Msimamo wa Bilal" au 'Bilal's Stand'. Filamu hiyo inasimulia maisha ya Bilal, kijana Mmarekani mwenye asili ya Afrika aishiye Detroit. Katika siku ya tatu hafla hiyo itakuwa na kikao cha 'Wanawake katika Uislamu'. Siku ya mwisho ya 'Wiki ya Kuufahamu Uislamu' itamhusu Suhaib Weeb, jambazi wa zamani aliyesilimu na sasa anajihusisha na harakati za Kiislamu.
Inatazamiwa kuwa hafla hiyo itatembelewa na wakazi wengi wa eneo hilo na kuinua kiwango chao cha kuufahamu Uislamu.
680724

captcha