IQNA

Misri yamzuia msomi wa Kishia kutembelea Iran

10:05 - October 24, 2010
Habari ID: 2018059
Maafisa wa usalama katika uwanja wa ndege wa Cairo Jumamosi asubuhi walimzuia Ahmad Rasem al-Nafis msomi, mtafiti, mwandishi na mwanafikra maarufu wa Kishia nchini humo kutembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa mujibu wa gazeti la Misri la Al Youm al Sabie, msomi huyo amezuiwa katika fremu ya sera za utawala wa Cairo wa kujaribu kukata uhusiano na maingiliano ya wasomi na wanazuoni wa Kishia wa Misri na wenzao wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Utawala wa Cairo umezidisha mashinikizo dhidi ya wasomi wa Kishia ambao ni wafuasi wa Ahlul Bayt (as).
Ahmad Rasem al-Nafis amewaambia waandishi habari kuwa, 'asubuhi ya leo nilikusudia kuelekea Dubai kisha nisafiri hadi Tehran lakini maafisa wa usalama katika uwanja wa ndege wa Cairo wamenipokonya pasi yangu ya kusafiria na kuniarifu kuwa siwezi kusafiri hadi Tehran'. Ameongeza kuwa, 'mimi nimealikwa na Taasisi ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (as) kushiriki katika kongamano la Umoja wa Kiislamu, lakini wakuu wa Misri bila kutoa sababu wamenipokonya pasi yangu na hivyo kunizuia kuwa na uhusiano na shakhsia wa kisiasa wa Kishia'.
Itakumbukwa kuwa serikali ya Uingereza pia imemzuia Ahmad Rasem al-Nafis kufika London kufuatia mashinikizo ya makundi ya Kiwahabi. 680659
captcha