IQNA

Misikiti 2,580 yajengwa na kukarabatiwa Tehran

12:05 - October 28, 2010
Habari ID: 2021112
Baraza la Mji wa Tehran ambo ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Tehran limedhamini ujenzi na ukarabati wa misikiti 2,580.
Kwa mujibu wa Mohammad Hadi Ayazi mkuu wa masuala ya utamaduni na kijamii katika Baraza la Mji wa Tehran, suala la kukarabati na kujenga misikiti ni kati ya majukumu muhimu ya baraza hilo.
'Mafunzo ya Kiislamu yanahimiza ujenzi na ukarabati wa misikiti', amesema afisa huyo. Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita Baraza la Mji wa Tehran limejenga misikiti 12 mikubwa na kuna mpango wa kujenge misikiti mingine 35 katika miaka ijayo.
Ameongeza kuwa kuna kumbi 1000 za sala ambazo zimejengwa katika mabustani, maduka makubwa, shule na vyuo vikuu.
683210
captcha