Akizungumzia suala hilo katika maonyesho ya kimataifa ya magazeti na mashirika ya habari yanayoendelea mjini Tehran, al-Mushrifi amesema akiwa katika kibanda cha Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA kwamba shirika hilo linatoa huduma kubwa ya Qur'ani kwa kusambaza duniani habari zinazohusiana na kitabu hicho kitakatifu kwa lugha 30 tofauti. Amesema shirika hilo linapaswa kuarifishwa ulimwenguni kuwa shirika kubwa zaidi la habari za Qur'ani.
Katika mazungumzo hayo, al-Mushrifi amegusia shughuli za Qur'ani zinazofanywa na Wizara ya Wakfu ya nchi yake na kuongeza kuwa hivi karibuni nchi hiyo itazindua Qur'ani ya Kitaifa iliyoandikwa kwa mkono na Salim al-Balushi, mwanakaligrafia mashuhuri wa nchi hiyo.
Amesema tayari Qur'ani hiyo imeshapitia hatua mbalimbali za uchapishaji na upambaji unaofanywa kwa makini na wasanii na wanakaligrafia wa Oman. 683982