Ripoti ya gazeti hilo imesema kuwa Sheikh Ahmad Tayyib atatembelea Iraq baada ya kuundwa serikali mpya na anatazamiwa kukutana na maraji’ na viongozi wa ngazi za juu ya madhehebu ya Shia wa Iraq akiwemo Ayatullah Ali Sistani.
Sheikh wa al Azhar pia atabadilishana mawazo na viongozi wa kidini wa Waislamu wa madhehebu ya Shia kuhusu njia za kukurubisha pamoja wafuasi wa madhehebu za Shia na Suni.
Safari ya Sheikh wa al Azhar nchini Iraq itakuwa sehemu ya maandalizi ya mkutano wa kimataifa wa maulamaa na wanafikra wa madhehebu za Shia na Suni. 684474