IQNA

Kikao cha kimataifa cha 'Nafasi ya Uislamu katika Ulaya Mpya' chaanza Ubelgiji

13:24 - October 30, 2010
Habari ID: 2021936
Kikao cha kimataifa cha 'Uislamu katika Ulaya Mpya' kilianza jana Ijumaa katika mji wa Antwerp nchini Ubelgiji.
Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO, kikao hicho kimeandaliwa na Chuo Kikuu cha Antwerp, Taasisi ya Sayansi za Kijamii ya Ibn Sina ya nchini Ufaransa, Jumuiya ya Kiislamu ya Ulaya, Jumuiya ya Kimataifa ya Wito wa Kiislamu WICS na Kitengo cha Utafiti wa Morocco na Mediterranean cha Chuo Kikuu cha Antwerp.
Mkuu wa Umoja wa Ulaya, wanachama wa Baraza la Ulaya, wawakilishi wa taasisi za kiutamaduni na kisiasa walio na hamu ya kufuatilia maudhui ya Uislamu barani Ulaya na vilevile watafiti walio na hamu ya kufuatilia suala la mazungumzo kati ya Uislamu na nchi za Ulaya wanashiriki katika kikao hicho.
Wawakilishi wa ISESCO pia wanashiriki katika kikao hicho kitakachomalizika hapo kesho Jumapili. Ubelgiji inaandaa kikao hicho kutokana na nafasi yake ya kuwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya. 684408
captcha