Kwa mujibu wa Idara ya Kitaifa ya Takwimu ya Uingereza Jina Muhammad , ukijumuisha namna mbalimbali linavyoandikwa, sasa ndio jina mashuhuri zaidi nchini Uingereza na limeyapita majina Oliver na Jack yaliyokuwa mashuhuri katika miaka iliyopita.
Khalid Anis, Msemaji wa Jumuiya ya Waislamu ya Uingereza amepongeza ripoti hiyo na kusema Waislamu nchini humo wanazidi kuielewa vyema dini yao. Ameongeza kuwa kutokana na Waislamu kuipenda dini ya Kiislamu, wengi sasa wanawapa watoto wao jina Muhammad.
Itakumbukwa kuwa mwaka 1944 jina Mohammad lilikuwa katika nafasi ya 87 kwa umashuhuri nchini Uingereza.
Sheikh Al Hasan, Imam wa Msikiti wa East London anasema jina Mohammad limepata umashuhuri kwa sababu wazazi wengi wanampenda Mtume Muhammad (saw) na wanajitahidi kumfuata katika maisha yao.
Idadi ya Waislamu nchini Uingereza inakadiriwa kuwa milioni 2.9.
685276