Kwa mujibu wa gazeti la Arab News, al-Farisi amegusia suala hilo alipokuwa akizungumza katika warsha ya mafunzo ya kudhibiti umati huko Jamarat Mina na kuongeza kuwa kwa kutilia maanani idadi kubwa ya mahujaji mwaka huu, hatua muhimu zimechukuliwa kwa ajili ya kuboresha hali ya mahujaji watakapokuwa wakirusha mawe kwenye daraja la Jamarat. Amesema warsha ya mafunzo ya Jamarat itakuwa ikifanyika kila mwaka kwa lengo la kubadilishana uzoefu na habari za kuboresha hali ya mahujaji na kurahisisha harakati yao wakati wa kurushia mawe mashetani huko Mina.
Al-Farisi amesisitiza kwamba Saudia ina nia ya kutekeleza miradi zaidi katika siku zijazo kwa madhumuni ya kuboresha hali ya mahujaji katika msimu wa hija. 685830