Kwa mujibu wa tovuti ya Wiki ya Kuufahamu Uislamu IAW, wiki hii huandaliwa kila mwaka nchini Uingereza kwa siku saba kuanzia Novemba mosi. Hafla za kuwafahamisha Waingereza kuhusu Uislamu huendelea kwa muda wa wiki moja katika miji mbalimbali ya Uingereza. Mwaka huu hafla za kuufahamu Uislamu zinazunguka katika mhimili wa Aya ya 13 ya Sura Hujurat ya Qur'ani Tukufu isemayo, 'Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari'.
Kwa kuzingatia kuwa wiki hii imesadifiana na msimu wa hija mwaka huu, waandalizi pia wameandaa mipango ya kuwafahamisha Waingereza zaidi kuhusu ibada ya hija. Jumuiya ya Kiislamu ya Uingereza ilianzisha hafla za 'Wiki ya Kuufahamu Uislamu' mwaka 1984 ili kuongeza ujuzi na kuondoa taswira potofu kuhusu Uislamu miongoni mwa Waingereza.
686823