Kongamano hilo ambalo litahudhuriwa na wataalamu wa masuala ya fedha na benki za Kiislamu litachunguza mbinu za kustawisha mfumo wa kifedha wa Kiislamu nchini Algeria.
Licha ya kwamba mfumo wa kifedha wa Kiislamu uliingia Algeria mwaka 1991 lakini hadi sasa mfumo huo una nafasi ndogo mno katika uchumi na biashara nchini humo. Kwa kuzingatia hayo kongamano la sasa la kitaifa la Uchumi wa Kiislamu litachunguza sababu za kutotiliwa maanani mfumo wa uchumi wa Kiislamu na mbinu zake za ustawi nchini humo.
Maudhui nyingine zitakazojadiliwa ni pamoja na uwekezaji katika sekta ya binafsi, mchango wa uchumi wa Kiislamu katika ustawi wa shughuli za kibenki na faida za soko la uchumi wa Kiislamu katika ustawi wa nchi. 687308