IQNA

Watu 210 wasilimu katika kipindi cha miezi miwili mjini Dubai

5:44 - November 04, 2010
Habari ID: 2025315
Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Dar al-Birr cha mjini Dubai, raia 210 wa mataifa tofauti wamesilimu na kuukubali Uislamu katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Kwa mujibu wa kauli ya Yusuf as-Said, mkuu wa kitengo cha upashaji habari cha kituo hicho, watu na familia zilizosilimu zinajumuisha raia wa nchi mbalimbali ambao wamevutiwa na utukufu pamoja na adhama ya mafundisho ya Kiislamu.
Amesema, kwa mujibu wa ratiba maalumu ambazo zimekuwa zikitekelezwa na kituo cha al-Birr tokea mwanzoni mwa mwaka hadi sasa, watu 110 wamefanikiwa kusilimu na kwamba kundi kubwa zaidi la watu waliosilimu lilishuhudiwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo watu 250 walisilimu kwa wakati mmoja.
Huku akiashiria kwamba maelfu ya watu walio na hamu ya kuufahamu Uislamu hukitembelea kituo hicho kila mwaka kwa hiari yao wenyewe, Bwana Said ameongeza kuwa watu hao hupewa zawadi ya vitabu vya maarifa na mafundisho ya Kiislamu ambavyo hukidhi hamu yao ya kutaka kuujua Uislamu.
Kituo hicho katika kipindi cha miaka 30 iliyopita kimekuwa kikijishughulisha na masuala mbalimbali ya kueneza Uislamu duniani, ikiwemo shughuli ya kuchapisha na kutarjumu kwa lugha tofauti hai za dunia vitabu vya Kiislamu. 687332
captcha