IQNA

Wanawake wa Saudia kuwa na chuo cha walimu wa Qur'ani

6:00 - November 04, 2010
Habari ID: 2025320
Taasisi ya kheri ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya mji wa Riyadh Saudi Arabia imeafiki kuanzishwa jumuiya ya kwanza ya kutayarisha walimu wa kuhifadhi Qur'ani makhsusi kwa ajili ya wanawake nchini humo.
Jumuiya hiyo iliyopewa jina la Kituo cha Mafunzo cha Qur'ani kitakuwa cha kwanza cha kutayarisha walimu wa kuhifadhisha Qur'ani cha wanawake nchini Saudi Arabia.
Yusuf al Mahus Imam wa mojawapo ya misikiti ya Riyadh ambaye amechaguliwa kusimamia kituo hicho amesema kuwa katika kituo hicho kutatolewa masomo ya jinsi ya kuamiliana na wanafunzi, kutoa maarifa ya Qur'ani, kutadabari ndani ya kitabu hicho na kuelewa mafundisho yake yenye thamani kubwa.
Ameongozea kuwa kituo hicho pia kitakaribisha shakhsia na wataalamu mashuhuri wa sayansi ya Qur'ani ambao watatoa hotuba kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na taaluma ya Qur'ani Tukufu.
Ameongeza kuwa masuala mengine yatakayojadiliwa katika kituo hicho ni kanuni za kutadabari katika Qur'ani, tafsiri ya aya za Qur'ani zinazohusiana na wanawake na kanuni na mbinu za kufasiri aya za Qur'ani. 687879
captcha