IQNA

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani Visiwani Comoro wazawadiwa

12:01 - November 04, 2010
Habari ID: 2025340
Washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika Visiwa vya Comoro wamezawadiwa katika hafla iliyofanyika Jumanne.
Kwa mujibu wa gazeti la Ash-Sharq sherehe hizo zilizofanyika katika majengo ya Bunge mjini Moroni zilihuduriwa na Spika wa Bunge la Comoro Borhan Ahmed na mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar Ahmed bin Muhammad Al-Merrikhi, Mkuu wa Waqfu wa Misaada ya Kibinadamu Qatar Ayez Al-Qahtani na mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu Abdullah Ma’ayuf Al-Jaeed.
Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu yaliandaliwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa himaya ya Waqfu wa Misaada ya Kibinadamu wa Qatar na Wizara ya Uadilifu na Masuala ya Kiislamu nchini Comoro.
Mashindano hayo yalikuwa katika vitengo vitano vya kuhifadhi Juzuu 5, 10, 15, 20 na kuhifadhi Qur'ani nzima.
Visiwa vya Comoro viko katika eneo la magharibi mwa Bahari ya Hindi yapata maili 200 kutoka pwani ya Afrika Mashariki. Nchi hiyo ina idadi ya watu wasiozidi milioni moja. Karibu asilimi 98 ya Wacomoro ni Waislamu.
687951
captcha