IQNA

Maonyesho ya vitabu vya miujiza ya kisanyansi katika Qur'ani Sharjah

11:49 - November 04, 2010
Habari ID: 2025342
Vitabu kuhusu miujiza ya kisayansi katika Qur'ani Tukufu vinaonyeshwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Sharjah.
Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Imarati WAM, vitabu hivyo viko katika kibanda cha Taasisi ya Kimataifa ya Tunzo ya Qur'ani ya Dubai. Mkuu wa taasisi hiyo Ibrahim Boumalha amesema vitabu vilivyo katika maonyesho hayo ni mjumuiko wa makala zilizowasilishwa katika Kikao cha Kimataifa Kuhusu Miujiza ya Kisayansi katika Qur'ani Tukufu kilichofanyika Dubai miaka mitatu iliyopita.
Amesema taasisi hiyo pia itaonyesha vitabu vya Kiislamu na vya miujiza ya kisayansi katika Qur'ani katika awamu ya 21 ya Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Abu Dhabi.
Maonyesho hayo ya Abu Dhabi yanahesabiwa kuwa ni maonyesho bora zaidi ya vitabu vya Kiislamu duniani.
Maonyesho ya 29 ya Kimataifa ya Vitabu ya Sharjah yalizanza Oktoba 26 na yataendelea hadi Novemba 6. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kati ya nchi zinazoshiriki katika maonyesho hayo.
687977
captcha