Kwa mujibu wa Muhammad Hussein Sabzali mkuu wa Kituo cha Darul Qur'an cha Imam Ali AS kinachoandaa mashindano hayo, washiriki wataweza kushindana katika viwango vitatu vya kuhifadhi Qur'ani Tukufu na vile vile Tarteel.
Amesema wanawake 160 watashiriki katika mashindano hayo ya siku tatu yatakayofanyika katika Kituo cha Kidini cha Fatimiyun mjini Tehran.
Kituo cha Darul Quran cha Imam Ali AS kimesema mashidano ya wanaume yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Disemba 29.
686500