IQNA

Washindi wa mashindano ya taifa ya Qur'ani ya Iraq watangazwa

14:47 - November 06, 2010
Habari ID: 2026370
Idara ya Wakfu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq imetangaza majina ya washindi wa mashindano ya tatu ya kitaifa ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya watu wenye vipaji.
Mwenyekiti wa Idara ya Upashaji Habari ya Darul Qur'ani ya haram ya Imam Hussein (as) Ammar al Khazai amesema kuwa mashindano hayo yalifanyika pambizoni mwa Tamasha ya Kimataifa ya Wiki ya Qur'ani mjini Karbala katika nyanja za tafsiri ya Qur'ani na kusoma kitabu hicho.
Ameema kuwa mashindano hayo yamehudhuriwa na wawakilishi wa mikoa mbalimbali ya Iraq. Amesema kuwa Badri Abbas, mwalimu wa tafsiri ya Qur'ani wa Darul Qur'ani ya Karbala ameshika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Tamasha ya Kimataifa ya Wiki ya Qur'ani lilifanya mwezi uliopita chini ya usimamizi wa haram ya Imam Hussein (as) na Idara ya Wakfu ya Shia ikishirikisha wawakilishi kutoka nchi 20. 689012
captcha